Talaka ya Jide Mazito Yaibuka!


Siku chache baada ya staa mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ kupewa talaka mahakamani na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’ mazito yameibuka baada ya kubainika uwepo wa hati nyingine ya talaka aliyoitoa Gardner kwa mwanamke mwingine, Risasi limeinasa.


Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa mbali ya Jide anayetarajia kuibuka na kishindo kikubwa cha mabadiliko ya muziki wake hivi karibuni, Gardner alimpa talaka mahakamani mkewe wa awali aliyefahamika kwa jina la Idda Pius Mkunja, mwaka 2003.

“Mwenzangu Gardner anaonekana ndiyo kamchezo kake kumalizia ndoa mahakamani, ukiachana na Jide nimeona hati ya talaka nyingine aliyoitoa kwa Idda ambaye alimuona mwaka 1997,” kilisema chanzo hicho huku kikimpenyezea hati hiyo ya talaka (tazama pichani) mwanahabari wetu.

Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Gardner na Jide walishindwana miaka michache tu baada ya kufunga ndoa lakini waliendelea kuishi kwa imani kwamba wanaweza kuelewana lakini haikuwezekana.

“Hii ishu si ya miaka miwili iliyopita kama wengi wanavyojua. Ndoa ilikuwa na figisu muda mrefu sana, walishashindwana sema walifanya siri tu,” kilisema chanzo.

Baada ya kupewa hati hiyo, mwanahabari wetu alimtafuta Gardner ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake iliita bila kupokelewa.

Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment


Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016