Dallas wa Jack Wolper Afunga Ndoa...


ALIYEKUWA mchumba wa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, Ramadhan Mtoro ‘Dallas’ inadaiwa kuwa hivi karibuni amefunga ndoa na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Suleiya, Amani lina mchongo kamili.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita maeneo ya Mbezi-Ununio jijini Dar ambapo wawili hao walionekana wakiwa katika hali ya furaha muda wote huku ndoa hiyo ikifungwa bila kificho.

“Hatimaye leo yamekuwa, yaani yule jamaa (Dallas) aliyekuwa akimpatia Wolper magari ya kifahari na mipesa leo hii saa saba mchana (Jumapili) anafunga ndoa tena na mwanamke mwingine mkali kuliko hata huyo Wolper,” kilisema chanzo.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Amani lilifanikiwa kutimba eneo la tukio na kushuhudia Dallas akifunga ndoa kweli na mwanamke huyo ambapo baadaye waliingia moja kwa moja kwenye gari na kutokomea.

Miaka mitatu iliyopita Dallas alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Wolper hadi kufikia hatua bi’dada huyo kubadili dini ili aolewe naye lakini mwishowe uhusiano huo uliyeyuka.

No comments:

Post a Comment


Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016