Shilole Ala za Uso, Atakiwa Kuacha Kubemenda Vijana Wadogo....


Msanii wa bongo fleva asiyeisha vituko Shilole au Shishi Baby, ameijiwa juu na mashabiki wake na kumtaka kuacha tabia ya kupenda wavulana wadogo, huku wakimtuhumu kuwabemenda na kujidhalilisha.

Kwenye ukurasa wake wa instagram ambapo Shilole amepost picha akiwa na mwenzi wake huyo mpya ambaye pia ni mwanamuziki Nedy Music, mashabiki hao wamemtaka Shishi kuacha mara moja kwani anawafundisha vibaya watoto wake ambao ni wakubwa.

ester_mbise : Mbona huo ni ubakaji sasa!! Kitoto kidogo sana hicho unakibemenda!!! Yaaaaan bora hata Nuh kdg japo naye alikuwa katoto!!! Daaaaaaaaah

janejoseph88.jj : acha kubeba watoto wadogo dada yangu hebu jiheshimu japo kidogo fikria kuwa na ww pia unamtoto wa kike hata kama unahela

anifamwakalobo : Jmn kumbe ndo style yako unapenda vitoto haaaa wewe mmama saiz zako huzioni mbona utamaliza kubemenda watoto wa wenzio!!! Huyo kijana ilifaa atoke na mtoto wako ww uwe mamamkwe daaa kweli hii dunia kuna watu na viatu ila wengine ni yeboyebo sasa,,, umezidi unatuzalilisha wanawake wenzio hiv unafikili wazazi wa huyo kijana watajiskiaje kwa mfano shilolekiuno???

lily_da_bae:This lil boy is being raped. This is so disgusting. Dating kids who are almost same age as your own kids. Hm!! Im sure this kid is broke n all he needs is $$$ but not true love. Look for a man if you want to be truly loved, otherwise you will date more than 100 of these kidos.

Akimaanisha....... (huyu mvulana mdogo anabakwa, hii inachukiza, kuwa na mahusiano na watoto ambao umri wao ni karibu sawa na watoto wako, hm, nina uhakika huyu mtoto amefulia na vyote anavyotaka ni dola na si mapenzi ya kweli. Tafuta mwanaume kama unataka kupendwa kweli, vinginevyo utatoka na zaidi ya 100 ya hawa watoto).

Hayo yameandikwa na mashabiki hao wakimtaka Shilole kuacha hiyo tabia ya kuwa na mahusiano na vijana wenye umri mdogo.

Hivi karibuni Shilole aliachana na mpenzi wake Nuh Mziwanda, ambaye pia alikuwa mdogo kwake kiumri.

4 comments:

  1. MBONA ZARI HAMUMSEMI AU NDO MNAMUOGOPA KWA KUWA NI BOSS LADY,? NA HAO VIJANA KWANI HAWAJIONI KUWA NI WADOGO? ACHENI KUJIFANYA MNAJUA UMRI WA WATU SANA KWANI MAPENZI HAYANA UMRI, VIKONGWE WANGAPI KWENYE NCHI ZETU HIZI ZA MABLACK WANAOA VIBINTI VIDOGO.??? MUMKOME SHISHI BABY.
    Reply
    Replies
    1. Wema na Idriss je ? Antie na Iyobo ??
  2. Je?Na dingi wa miaka 50 au zaidi akimla uroda binti wa miaka 18 hiyo ni halali au?Maana hata sielewi elewi ifahamikavyo kisheria mtu akifikisha umri wa miaka 18 anahesabiwa kisheria kuwa ni timamu sasa kama tujuavyo mapenzi huwa hayana umri rangi wala kabila sema sisi walimwengu huwa tunalitolea sana mapovu haswa pale demu anapokuwa mkubwa kiumri kumzidi mwanaume wake oh too much bla bla here too bla bla there lakini ikiwa dingi mwenye umri mkubwa na kabinti kinakoweza kuwa umri sawa na binti yake oh hapo waswahili mnasifia yaani sielewi which is which and what is what kudadeki
    Reply
  3. Wanawake tu ndio wanabemenda watoto wanaume je? Acha wale ujana,,,,
    Reply

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 4 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016