Ray Kigosi Akana Katu Katu Kuwa Anajichubua Ngozi...Adai Anafanya Mambo yafuatayo Mpaka Ngozi yake Inakuwa Nyeupe


Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Ray Kigosi amesema kwamba yeye hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi .
Ray ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV na kusema kwamba hua anakwenda salon mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.
Naye Mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba Mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.
Katika kipengele cha ''Cheche'' ambacho majirani hupewa nafasi ya kumzungumzia msanii au mgeni wa siku kwenye show wamesema kwamba Ray apunguze kutumia vipodozi kwani anakuwa kama mchina.
Pia wamemtaka mwigizaji huyo kuwa na moyo wa kusaidia wasanii chipukizi ilikukuza tasnia ya uigizaji hapa nchini.

1 comment:

  1. hawi kama mchina bali anakuwa kama demu ama zaidi ya damu anaetafuta bwana
    Reply


Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu