Polisi Yavamia Harusi, Wakamata Bwana Harusi na Watu Wake Kwa Kuhusishwa na Kesi ya Ujambazi Access Bank
Baada ya kupitapita huku na kule katika maeneo yaliyotokea kadhia ya ujambazi jana nilifanikisha kunasa tukio Moja maeneo ya Chulwi Kongowe Mbagala kama sijakosea.Mnamo 27.2.2016 majira ya SAA 12 jioni polisi walivamia harusi iliyokuwa ikifungwa msikitini na kuwakamata watu waliokuwemo ndani wakiwatuhumu kuhusika na Ujambazi uliofanywa siku ya tarehe 26.2.2016 katika tawi moja la Bank ya Access lililoko Mbagala.Raia walisema polisi ilivamia msikiti na kuwakamata walimu wa dini waliokuwa wakifungisha ndoa hiyo na kuwachukua na kwenda nao hadi ilipo harusi na kuwakamata wengine huku wakiwapiga na kuwatuhumu kuwa wamehusika na ujambazi.Hata hivyo polisi ilimwachia huru bibi harusi na kuondoka na babu harusi na wapambe wake sehemu kusiko julikana.Miongoni mwa watu waliokamatwa ni Abdullah Saudi, Juma selemani, Saidi Ally na kassimu Othuman wote wakiwa wakazi wa Mbagala waliokuja kusheherekea harusi ya rafiki yao.
Comments
Post a Comment