AY Awashangaa TCRA kwa Kuifungia Video ya zigo Remix..Alichosema Kiko Hapa.


Baada ya kuwepo taarifa kuwa video ya A.Y,Zigo aliyomshirikisha Diamond imefungiwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kutokana na kutokuwa na maadili,msanii huyo amekiri kupokea barua kutoka kwa mamlaka hiyo.

Hata hivyo AY ameshangaa hatua hiyo na kuhoji ni maadili yapi ambayo hayajazingatiwa kwenye video hiyo,na pia mbona hawafungii video za nje ambazo zinakiuka maadili zaidi.

“Unajua unavyo shoot una shoot kama maudhui ilivyo,huwezi ukavaa suti jangwani au ukavaa overall kwenye swimming pool..na mavazi ya swimming pool yako kila sehemu hata katika taarifa ya habari tunayoona kwenye vipindi vya michezo kama wao pia wanakiuka habari nitakubaliana nao..kama wanafungia wimbo wa zigo na kuacha za kina nick minaj ni sawa kama wanaona maadili ya kina Nick Minaj yako sawa na kina Ay ndo mabaya,inabidi kukubaliana nao” alifunguka Ay

Hata hivyo Innocent Mungi kutoka TCRA hakutaja moja kwa moja kuwa video hio umefungiwa bali wametoa barua kwenda kwa vituo vinavyorusha matangazo ya Tv kuwa wasimamie kanuni za maudhui ya utangazaji kusitisha kurusha nyimbo zote zinazokiuka kanuni hizo

Post a Comment


Emoticon

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016