Dogo Janja Aikana Sauti yake Akimtongoza Msichana na Kuwaponda Tip Top...Madee Amtetea Asema Utoto Unamsumbua...


Rapper Dogo Janja ambaye kwa sasa yuko chini ya uongozi wa Tip Top  ameikana sauti iliyosambaa mitandaoni inayodaiwa kuwa ni yake akiwa anamtongoza msichana na kusikika akiu diss uongozi wa Tip Top kuwa unambania(soma hapa)

Dogo Janja alipoulizwa na kituo kimoja cha redio kuhusiana na sauti hiyo alikataa na kusema hajui chochote kuhusiana na swala hilo mpaka afuatilie.

Hata hivyo Madee alipoulizwa kuhusiana na sauti hiyo akasema ameisikia lakini ameigundua ni mambo ya kitoto ya dogo Janja pengine aonekane ana sauti kwa huyo binti aliyekuwa anamtongoza.

“Nimesikiliza nimeona mambo ya kitototo ndo maana hata sijataka kuhangaika nayo sana,nilichogundua ni kwamba alitaka kujionyesha anaweza kuongea kwa sauti yoyote kwa mwanamke lakini kama Tip Top tutakaa tutajua nini cha kumwambia” alifunguka Madee na kuweka wazi kuwa ngoma mpya ya dogo Janja itatoka mwisho wa mwezi huu.

1 comment:

  1. Safi sana Madee. Hata km ningekuwa mimi natafuta kiki kwa huyo dem. Ningeponda ila akili kichwani. Kumbe dem jenyewe linapenda nyimbo na sio Dogo janja. Lika eneza Sauti hiyo ili lipate kiki. Mchukulieni poa Dogo mmtoe. Tunapotongoza huwa tunasema mengi sisi wanaume achetu. kunawatu huwa wanadiliki kusema wana Hisa asilimia 45 Vyamkom. Yote kutafuta kiki akivuliwa chupi kaisha.
    Reply


Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016