Mtoto wa Kanye West Amchanganya Wema Sepetu.....
Wema Sepetu jana amepost picha zaidi ya tatu Instgram za mtoto huyo huku akionesha ni jinsi gani ametokea kumpenda mtoto huyo na kudai ni mzuri sana, lakini haikuishia hapo Wema Sepetu aliamua kuweka picha hiyo kwenye Profile yake Instgram na kuweka picha hiyo kama Wall Paper na Screen save kwenye simu yake.
“Gnyt now… But Kimberly Kardashian sio kwa mtoto mzuri hivi jamani. Kama Pipi…!!! Mashallah jamani… God…! You are Able…! Saint West mzuri mno jamani… Dis Baby Boy too pretty ooo” Aliandika Wema Sepetu.
Kutokana na kitendo hicho mashabiki wa Wema ambao wanafahamika kama Team Wema walianza kumfariji Wema na kumpa maneno yenye faraja na yenye kumtia moyo kuwa ipo siku na yeye atapata mtoto, kwani Mungu ndiye anapanga kila jambo.
“Mungu hutoa kwa wakati wake na kwa sababu zake. Kama alivyowaona wengine na wewe atakuona hivyohivyo. Naatakupa haja ya moyo wako. Mungu tu ndio atakae weza kukusaidia my dear wema. Worry out your time will come soon keep on hoping that I love u.” Aliandika Hoperitha Minja
“Usijali iposiku utakuja kuzaa na mwanaume wa furaha yako ulio mpenda na yeye akakupenda, ninavyo kupenda kama mtanzania mwenzako kilasiku nakuombea kwa Mungu akupe afya na maisha marefu uzidi kututungia kazi nzuri na zitambulike dunia nzima I love you Wema” Aliandika king._of_ma_love_davi
Ingawa si watu wote walipendezwa na maneno ya Wema Sepetu kumsifia mtoto huyo ndipo hapo aliwaamsha watu ambao wamezoea kumtolea maneno machafu na wanaotumia lugha chafu na za kuudhi si kwake tu bali hata kwa watu waliostaarabika na watu wenye utu, kwani wasingweza kutumia maneno ambayo wanajua wazi yanaweza kuumiza wengine.
Emoticon