Skip to main content

Video: Sauti Sol waonyeshwa kuchukizwa na rubadi anaye adaiwa kumdhalilisha polisi wa kike Kenya


Kupitia account yao ya Facebook, Kundi la muziki la Sauti Sol kutokea nchini Kenya wameonyeshwa kuchukizwa na rubani wa ndege aliye mzalilisha polisi wa kike nchini humo. Sauti Sol wameandika "We welcome you to our beloved country, treat your as a brother and this is the thanks we get? A fully grown man assaulting our law enforcement officer, moreso a woman? ‪#‎LiveandDieinAfrika‬"



Rubani adaiwa kumdhalilisha polisi wa kike Kenya

Polisi nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa ambapo rubani wa ndege iliyombeba Naibu Rais William Ruto anadaiwa kumdhalilisha afisa wa polisi wa kike.
Kisa hicho kilitokea Jumapili wakati Bw Ruto alikuwa amezuru mji wa Ndunyu Njeru, jimbo la Nyandarua katikati mwa nchi hiyo.

Video iliyochukuliwa na mmoja wa walioshuhudia kisa hicho imesambaa sana mtandaoni watu wakitaka hatua zichukuliwe dhidi ya rubani huyo.
Kwenye video hiyo, rubani huyo anaonekana akimkaripia mwanamke huyo ambaye wakati huo anatumia simu, kumpokonya bakora yake na kicha majibizano yanatokea. Muda mfupi baadaye, rubani huyo anaonekana akimsukuma afisa huyo wa polisi.

Mkuu wa polisi Joseph Boinnet, kupitia taarifa, ameagiza maafisa wa polisi kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusu kisa hicho na pia akamtaka rubani huyo kujisalimisha kwa polisi.

Afisa wa mawasiliano wa Bw Ruto, Bw David Mugonyi, amesema kiongozi huyo amefahamishwa kuhusu kisa hicho.

“Naibu Rais amewaagiza polisi kuchukua hatua mara moja. Naibu Rais anaheshimu polisi wetu wenye bidii ambao hufanya kazi saa nyingi kulinda nchi. Kisa hiki hakikubaliki, na ni cha kusikitisha na nimewataka polisi kuchunguza kitendo hicho cha rubani huyo,” taarifa yake imesema.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016